Wednesday, May 15, 2019

DARASA LA RAMADHANI

Bismillahi Rahmani Rahim. Karibuni wenzangu waumini wa kiislamu katika kipengele hiki kitachoelezea namna mama mjamzito na mama mnyonyeshaji mtoto watafunga Ramadhani yao.


✍🏼 Eleweni enyi wenzangu kwamba, mwanamke mja mzito huwa hapati hedhi hivyo ni wajib kwake kufunga,  Lakin pia mwenye kunyonyesha mtoto wake nae kama hayupo katika hedhi au nifasi ni wajib kwake kufunga.

👉 Lakini sasa , wawili hao wakichelea/wakihofia kwamba wakifunga watadhurika wao au wao na vitoto vyao vichanga basi hawatoruhusiwa kufunga , na watakuja kulipa swaumu zilizowafutu Siku zijazo baada ya mfungo .

👉 watalipa swaum ikiwa wamehofia madhara katika nafsi zao tu, na watalipa fidia pia kama  itakua wamehofia madhara ya vitoto vyao vichanga . fidia hiyo ni kumlisha maskin au fukara mmoja kwa kila siku moja ambayo mtu hakufunga atamlisha maskini mmoja .

Allahu Aaalamu .

Katika kipemgele hiki tutizame namna gani mtu mzee yani Mtu mzima atatekeleza ibada ya swaum.

Mimi nawaomba muelewe enyi wenzangu wasaka Pepo ya kwamba, mtu yoyote mwenye kushindwa kufunga kwa sababu ya uzee anaruhusiwa asifunge na hatolipa swaumu Bali atatoa fidia tu ya kumlisha maskin mmoja ya kila siku ya Ramadhan.

Allahu Aaalamu .

✍🏼. Hadi hapo tuweke nukta.
☝yafahamuni vyema hayo

*WASAKA PEPO* (2019)

No comments:

Post a Comment

 
back to top