Wednesday, May 15, 2019

KAFARA LA KUFANYA TENDO LA NDOA KATIKA MCHANA WA RAMADHANI

Bismillahi Rahmani Rahim,

*KAFARA LA KUFANYA TENDO LA NDOA KATIKA MCHANA WA RAMADHANI*

✍Nawaomba mfahamu enyi wenzangu kwamba, kufanya tendo la ndoa kwa hiyari katika
mchana wa Ramadhani ni katika madhambi makubwa sana. Na sheria itamtaka mwenye kufanya
hivyo atoe kafara kubwa baada ya mfungo kuisha na kafara hiyo ipo katika utaratibu huu ufatao.

1)Kuacha mtumwa awe huru, hilo likishindikana afanye lifatalo.....
  •  Kufunga siku sitini kwa mfululizo ila ikitokea dharula kama ya maradhi hatofululiza dharula
ikisha isha ataendelea pale alipoishia . na mtu mtoa kafara hiyo akisitisha bila dharula ya
kisheria itabidi aanze upya kufunga hizo siku sitini kwa mfululizo. Ikishindikana hivyo atafanya
hili lifatalo
  • kulisha masikini sitini kila mmoja 2.5kg cha chakula kinacholiwa Mara nyingi katika jamii
husika . lazima wawe masikini 60 tofaut kila mmoja kibaba chake hilo lifanyike kwa siku 60. Na
kwa kila siku moja utoe 2.5kg za chakula kwa maskini husika.

*MAELEZO YA ZIADA*
Kulipa kafara hiyo kuna ambatana na kulipa swaumu ya ile siku ambayo mtu alifanya tend
la ndoa katika mchana wa Ramadhani.
Ikiwa mwanamke kalazimishwa kufanya tendo la ndoa , hatolipa kafara atalipa swaumu tu
Lakin kama huyo mke naye alichochea kufanyika kwa tendo la ndoa mchana wa Ramadhani
atapaswa nae atoe kafara.
Wanandoa ambao ni wasafiri na hawakufunga na mtu ambaye amefanya tendo la ndoa kw
kujisahau , au ambaye alikua afahamu uharamu wa kufanya tendo la ndoa mchana wa
Ramadhani

Watu hao wakifanya tendo la ndoa mchana wa Ramadhani hawatalipa kafara Bali watalipa
swaumu tu .
Allahu Aaalamu.
Yafahamuni vyema hayo ☝
✍Hadi hapo tuweke nukta

*WASAKA PEPO* (2019)
RAMADHAN KAREEM.

No comments:

Post a Comment

 
back to top