Wednesday, May 15, 2019

SAWALA ZA USIKU

Basi Hili ni somo kuhusu swala za usiku, litakuwa katika sehemu 3

*SEHEMU YA KWANZA NI KATIKA KUZUNGUMZIA QIYAAMULLAYLI*
Fahamuni enyi wenzangu kwamba Qiyaamullayl ni swala ya sunnah yoyote inayoswaliw
usiku baada ya kuswali swala ya isha(swala ya sa mbili usiku) . Kisha fahamuni tena kwamba
idadi ya rakaa kwa swala hiyo ya qiyaamullayl ni rakaa mbili kisha watoa salamu. Hapo
namaanisha kwamba waweza swali rakaa zozote utakazo lakini kwa utaratibu wa kwamba
waswali rakaa mbili kisha watoa salamu alafu tena mbili kisha watoa salamu hadi pale
utapotimiza idadi ya rakaa ulizokusudia kuziswali.
Mfano wa Qiyaamullayli ni swala ya tarawehe.
Pia fahamu kuwa Qiyaamullayl waweza lala kwanza kisha ndo ukaamka kuiswali au waweza
iswali kwanza kisha ukalala.

*SEHEMU YA PILI NI KATIKA KUZUNGUMZIA TAHHAJUD*
✍Tahajjud ni aina ya Qiyaamullayl
yenye sifa moja kuu iliyo yamsingi.
Na sifa hiyo kuu ni kwamba tahajjud ni qiyaamullayli ambayo huswaliwa baada ya mtu kulala
kisha aka amka.
na hadi hapo tujikite katika sehemu ya tatu na ya mwisho inayohusu swala ya witri.

*SEHEMU YA TATU INAELEZEA KUHUSU SWALA YA WITRI*
Swala ya witri ni swala ambayo huswaliwa baada ya mtu kumaliza swala zake za usiku.
Witri inaweza swaliwa rakaa 1, 3 , 5, 7, 9 , 11.
Ukiiswali kwa rakaa tatu, utaswali mbili kisha utatoa salamu , alafu utasimama umalizie moj
ili ziwe tatu.
Ukiiswali kwa rakaa zozote zile katika hizo rakaa tulizotaja utaswali mbili mbili kisha moja y
mwisho utaiswali kivyake .
Pia katika rakaa ya mwisho ya swala hiyo ya witri ni vyema uombe dua ya qunuti ambayo
huombwa pindi unapotoka kurukuu sasa ukiwa umesimama wima kabla ya kusujudu, utaiomba
dua hiyo ya Qunuti ambayo nitaileta kwenu .

Twab-an.
Ndio kama hivyo. Na utaratibu wa swala zote hizo tulizozizungumzia ni kama ulele wa swal
nyingine yani swala tano za faradh kwa kuzingatia nguzo na masharti kama vile kuwa na udhu,
kuelekea qibla nakadhalika.
Na kwa hakika kuna thawabu, malipo na fadhila nyingi sana katika kuziswali swala za usiku
pamesemwa na waja wema kwamba swala hizo ni kifunguo cha kila kheri na kukubaliwa dua.

✍ Mpaka hapo tulipo fikia, nasema Allahu Aalamu, Assa laamu alaykum Warahmatullahi
Wabarakaatuhu.

Wasaka Pepo (2019)

No comments:

Post a Comment

 
back to top