Wednesday, May 15, 2019

MAAJABU 10 YA MCHANGANYIKO WA TENDE NA MAZIWA

BISMILAH RAHMAN RAHIM

HAYA NDIYO MAAJABU KUMI ( 10 ) YA MCHANGANYIKO WA TENDE NA MAZIWA

Karibu Katika Makala hii Mahususi Ya Lishe Bora ambayo leo inakuangazia Umuhimu wa Juisi
ya Mchanganyiko wa TENDE na MAZIWA - Vyakula hivyo vinapoliwa kwa pamoja huwa ni
sawa na ‘dozi’ matata yenye kuwaongezea makali ya kuridhiana kinyumba baina ya wanandoa (
Mke Na Mume ).
Aidha, tende na maziwa huwa na uwezo pia wa kuwaondolea walaji uwezekano wa kupata
maradhi mbalimbali yakiwamo ya saratani na chanzo cha kuwa na uwezo huo ni wingi wa
virutubisho vinavyopatikana ndani ya mchanganyiko wa vyakula hivyo.

UNDANI WA MAAJABU 10
Kwa pamoja, baadhi ya virutubisho muhimu vinavyopatikana ndani ya mchanganyiko w
vyakula hivyo ni pamoja na vitamini B1, B2, B3, B5, A1 na C.
Vingine ni Calories (nishati) na madini yakiwamo ya Calcium, Potassium, Magnesium,
Phosphorous, kiinilishe cha Folate na pia wanga.
Mambo 10 ya faida yanayoweza kupatikana kwa ulaji wa mchanganyiko kama juisi ya tend
na maziwa kuwa ni pamoja na :-

MOJA
Kuwaongezea nguvu na ubora wa mbegu wanaume walio na tatizo hilo.
PILI 
Kuinua hamu na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa kina mama; tatu kuimarish
afya ya mama mjamzito na kichanga chake.
NNE
Uwezo wa kusaidia kuondoa vilevi mwilini (hasa kwa wanywaji pombe).
TANO
Uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya magonjwa kama saratani ya tumbo na kiharusi.
SITA
Kusaidia mchakato wa usagaji wa chakula tumboni.
SABA
Faida ya mchanganyiko huo kuondoa tatizo la ukosefu wa choo au mtu kupata cho
kigumu.
NANE
Uwezo wa kumuondolea mtu uchovu.
TISA
Kuongeza damu mwilini kutokana na kujaaliwa wingi wa madini chuma
KUMI
Uwezo wa kusaidia mishipa ya fahamu kufanya kazi yake vizuri.

Wanasayansi mbalimbali duniani wamebaini uwezo wa mchanganyiko wa tende na maziwa
katika kuupa mwili lishe muhimu na hivyo ni vyema kila mmoja kula vyakula hivyo kwa ajili ya
kuimarisha afya yake bila kujali jinsia.

Tende ina protini na hivyo faida hiyo huwa maradufu zinapoliwa kwa kuchanganywa na maziwa
ambayo pia yana protini kwa wingi.

Tende zina kiasi kidogo cha mafuta yasiyo na rehemu na protini yake inapokuwa na maziwa
huwasaidia watu wote , Yaani wanawake na wanaume, hasa katika masuala ya afya ya uzazi.
Mchanganyiko wa vyakula hivyo huwasaidia wajawazito kwa sababu huwa na madini ya chuma
kwa wingi na mjamzito anapotumia humfanya kuwa na kiasi cha damu cha kutosha na
mwishowe kuzaa salama na kuwa mwenye afya njema.

“Mchanganyiko huu humrahisishia mjamzito kuzaa salama kwa sababu tende ina sukari
ambayo huwapa nguvu wajawazito katika kusukuma mtoto wakati wa kujifungua… bila nguvu
uzazi huwa mgumu,” .

Tende husaidia kuondoa tatizo la ukosefu wa choo au mtu kupata choo kigumu kwa sababu
tunda hilo limejaaliwa kuwa na nyuzi nyuzi (fibers) ambazo husaidia uyeyushaji wa chakula na
hilo hufanyika vizuri kwa kula na maziwa.

“Pia huondoa uchovu mwilini kwa sababu ina virutubisho vya sukari asilia kama glucose,
sucrose na fructose,” .

Madini ya potassium yaliyomo ndani yake husaidia kumwepusha mtu na maradhi ya kiharusi na
ina kiasi kidogo cha chumvi ambayo husaidia kuimarisha mishipa ya fahamu.

“Tende husaidia kupunguza lehemu mwilini na kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa
kukauka damu mwilini tende inaweza kuwapa ahueni kubwa,”.

“Tende ina vitamin A ambayo husaidia uoni mzuri na kuukinga mwili na maradhi, pia ina madini
ya chuma ambayo kazi yake ni kuzalisha chembechembe nyekundu za damu na ndiyo maana
zinapoliwa na maziwa huwa na msaada mkubwa kwa wajawazito.

MAANDALIZI.
Mchanganyiko wa tende na maziwa huweza kuandaliwa kwa namna nyingi na mojawapo ni
kuchukua tende zilizoiva kiasi cha kujaa kiganja kimoja cha mkono, kuondoa kokwa zake kisha
kuchanganya na glasi ya maziwa mabichi (fresh) kulingana na mahitaji.
Baada ya hapo, mchangayiko huo usagwe kwa pamoja ili kupata rojorojo kama juisi nzito
inayoweza kunywewa au kuwekwa kwanza kwenye friji ili ipate baridi kiasi Kidogo sana kabla
ya kutumiwa Ili Kufanya radha nzuri wakati wa Kutumia - Ujumbe huu nimeutayarisha

Mahususi Kwa ajili ya Kipindi hiki Cha Mwezi wa Ramadhani ambao Ndani yake Bidhaa Hii ya
Tende hupatikana Kwa Wingi Sana Na Si Mbali Na Maeneo tunayoishi , Tujitahidi Kudumu
Kwenye Matumizi ya Vitu Vya Asili ili kulinda Afya Zetu.

No comments:

Post a Comment

 
back to top