Wednesday, April 17, 2019

FAIDA ZA KUNYWA MAJI KATIKA MWILI


FAIDA ZA KUNYWA MAJI KATIKA MWILI

1: Kupunguza uzito: Kunywa maji mengi kunasaidia kupunguza uzito, kwani maji hayana
mafuta, kalori wala sukari.

2: Afya ya moyo: Unywaji wa maji mengi kunaweza kupunguza hatari ya kupatwa na ugonjwa
wa moyo. Utafiti wa miaka sita uliofanywa Marekani umeonesha kuwa watu wanaokunywa glasi
za maji zisizopungua 5 kwa siku, hujiepusha na uwezekano wa kupatwa na ugonjwa wa moyo
kwa asilimia 41 zaidi ya wale wanaokunywa glasi 2 au chini ya hapo.

3: Nishati ya mwili: Mwili unapopungikiwa maji, hukufanya ujisikie mchovu, hivyo kwa kunywa
maji ya kutosha daima utakuwa mwenye nguvu. Pendelea kunywa maji badala ya vinywaji
baridi kama soda, juisi au bia.

4:Tiba ya kichwa: Dalili ya mtu kupungukiwa maji mwilini ni pamoja na kuumwa kichwa. Kunywa
maji ya kutosha na hutasumbuliwa sana na kuumwa kichwa mara kwa mara.

5:Ngozi nyororo: Unywaji maji ya kutosha kila siku unaweza safisha ngozi yako na kuifanya
ionekane nyororo.

6: Matatizo ya choo: Maji ni dawa ya kutibu ukosefu wa choo, kunywa maji ya kutosha kila siku
na utajiepusha na tatizo la ukosefu wa choo mara kwa mara.

7: Usafishaji wa mwili: Maji husaidia kuondoa sumu mwilini kwa kutoa uchafu wote kwa njia ya
mkojo na haja kubwa.

8: Saratarani: Utajiepusha na saratani ya tumbo kwa kunywa maji, kwani maji husaidia suala la
usagaji wa chakula tumboni na hivyo wakati wote tumbo lako litakuwa safi. Utajiondoa katika
hatari ya kupata saratani ya tumbo kwa asilimia 45 na asilimia 50 kwa saratani ya kibofu cha
mkojo.

9: Mazoezi: Mwili unapokuwa na maji ya kutosha, yatakufanya uwe na nguvu ya kufanya
mazoezi yako ya kutosha, hivyo kupata faida ya mazoezi ipasavyo.

No comments:

Post a Comment

 
back to top