Wednesday, April 17, 2019

NAJISI

NAJISI (uchafu)
ni kitu chochote ambacho ni kichafu na hakifai katika mwili wa binadamu
AU  ni kila kitu ambacho kikiingia katika maji machache kinatenguwa uwezo wa kuyatumia maji hayo katika udhu/kujitwaharisha
Mfano wa najisi:-
  1. Damu
  2. Usaha
  3. Matapishi
  4. Udenda
  5. Choo kidogo na kikubwa
  6. Mzoga wowote isipokuwa wa binadamu,samaki na nzige
  7. Maziwa ya mnyama aliyeharamishwa kuliwa
  8. Pombe za aina zote
  9. Mbwa na nguruwe na kila kinachotokana nao
AINA ZA NAJISI
  1. NAJISI NZITO/KUBWA
  2. NAJISI YA KATI NA KATI/HAFIFU
  3. NAJISI NYEPESI/NDOGO
NAJISI NZITO
 Namna ya kujitwaharisha kutokana na najisi ya mbwa na nguruwe kuiosha sehemu hiyo mara saba na mojawapo katika hayo makosho saba iwe kwa kusugua kwa udongo safi.
 
NAJISI HAFIFU
Ni mkojo wa mtoto wa kiume ambaye yupo chini ya miaka miwili ambae hajaanza kula chakula ila maziwa ya mama tu.
Najisi hii hutwaharishwa kwa kumwagiwa maji tu sehemu iliyonajisika bila kusugua

NAJISI NDOGO
Najisi hii inahusu najisi zote isipkuwa najisi ya mbwa na nguruwe
Namna ya kujitwaharisha najisi ndogo ni kuosha palipo najisikikakwa maji safi mpaka iondoke rangi na harufu ya najisi.
MUHIMU:
Kama utatumia maji machache ambayo huharibika mara tu yatakapoingiwa na japo tone la najisi hatuna budi kutumia kata au chombo kingine cha kuchotea maji na kujitwaharisha pembeni kwa kujimiminia maji kupitia sehemu ile yemye najisi mpaka najisi hiyo iondoke.

No comments:

Post a Comment

 
back to top