Wednesday, April 3, 2019

TWAHARA

TWAHARA
 ni jambo lolote ambalo ukilifanya litaleta uhalali wa wewe kufanya ibada

ZANA ZA KUJITWAHARISHA
  1. Maji 
  2. Mchanga
  3. Kitu chochote chenye kuambua
  4. Mawe 
MATENDO YA KUJITWAHARISHA 
  1. Kushika udhu
  2. Kuoga jasho
  3. Kutaya mmamu 
  4. Kuondosha najisi 
KATIKA SHERIA KUNA MAELEZO YA MUHIMU KUHUSU MAJI
  1. Maji machache
  2. Maji mengi
MAJI MACHACHE 
Ni yale maji ambayo ujazo wake ni chini ya Lita 500 au chini ya ujazo wa pipa moja
         kwa mfano:- Maji ya kwenye ndoo
MAJI MENGI
Ni yale maji ambayo ujazo wake ni kwanzia Lita 500 na kuendelea au ujazo wa pipa na kuendelea
       kwa mfano:-
  1. Maji ya pipa
  2. Maji ya baharini
  3. Maji ya mtoni
SIFA ZA MAJI YANAYOFAA KUJITWAHARISHA 
  1. Maji ya mvua,mto,ziwa,bahari,theluji au chemchem   
NB: Yasiwe maji yanayotokana na matunda kama vile madafu,tikiti,marashi n.k
  • Yasiwe yamebadilika rangi,harufu au ladha
NB: Maji ya mchuzi au yaliyo na sabuni hayawezi kutwaharisha
  • Yasiwe yameshatumika kabla kujitwaharishia au kuondosha najisi
  • Yasiwe yameingiwa na najisi yoyote ile

1 comment:

 
back to top