Thursday, April 25, 2019

MAFUNZO KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Katika kipengele hiki twajifunza siku iitwayo siku ya shaka

✍�� Siku ya shaka ni ile siku ambayo ilitarajiwa iwe ndio siku ya mwanzo ya mwezi mtukufu w
Ramadhani kwa kuonekanwa mwezi siku ya nyuma tale lakini ikawa sio siku ya Mwanzo wa
Ramadhani kwa kuto onekana mwezi siku ya nyuma yake.
�� kwa maneno yaliyo mepesi kueleweka twaweza sema siku ya shaka ni île siku ya tarehe 3
ya mwezi wa Shaban.

*JEE YAFAA KUFUNGA KATIKA SIKU HIYO YA SHAKA ?*
�� Haifai na ni haramu mtu kufunga katika siku ya shaka . Pia ni haramu kufunga siku ya nyum
kabla yake.
�� Lakini itakua sio haramu kufunga katika siku ya shaka na siku ya nyuma kabla yake ikiw
siku hizo zitakua zimeangukia katika utaratibu wa funga za sunnah za mtu ambao mwenyewe
alikua akiufata . Mathalan funga ya Jumatatu na Alhamis Au funga ya masiku meupe na meusi.
�� Hivyo basi sio haramu kufunga katika siku ya shaka ikiwa tarehe ya siku hiyo ya shaka it
angukia katika siku za sunnah kufunga kama sunnah ya Alhamis, Jumatatu na nyinginezo.

Allahu Aaalam. Tuweke nukta hapo hadi badae tutapo ona kipengele kingine chenye mafunzo
ya dua ya mtu kusoma wakati mwezi wa Ramadhani unapo andama.
Allah atufanyie wepesi.

IMEANDALIWA NA AMIRI WA TAASISI YA WASAKA PEPO .
MUBARACK HASSAN CHIZENGA.

No comments:

Post a Comment

 
back to top