Monday, April 22, 2019

SALA YA MSAFIRI 2/4

*KUKUSANYA KWA KUTANGULIZA*

Kwa Maana Kuisali Adhuhuri na Laasiri ndani ya Wakati wa Adhuhuri
Au
Kuisali Magharibi na Isha Ndani ya Wakati wa Magharibi

*SHARTI ZA KUKUSANYA KWA KUTANGULIZA NI 7.*
*1.* Kuanza Kusali Ile Sala ya Mwanzo.
Mfano Utasali Adhuhuri kisha Laasiri.
*2.* Kuihudhurisha (Kuileta) Nia Katika Sala ya Mwanzo.
*3.* Ubakie Wakati wa Sala ya Mwanzo.
Yaani Uweze kuzisali sala zote mbili katika Wakati na Bado iwe Wakati haujamaliza.
*4.* Kuzifuatanisha.
Yaani Usali ya kwanza Bila ya kupita Muda Usimame kusali ya Pili.
(Usirefuke Muda Baada ya kumaliza Sala ya Mwanzo na kabla ya kuanza ya Pili).
*5.* Uwe na Dhanna Ya Kusihi kwa Sala ya Mwanzo.
Usiwe na Shaka juu ya kusihi Sala ya Mwanzo.
*6.* Udumu Udhuru wako Mpaka Utakapo kamilisha Takbira ya Kuhirimia Sala ya Pili.
*7.* Uwe na Elimu ya Kujuzu Kuchanganya Sala.

*.........................................................*
*2/4*

No comments:

Post a Comment

 
back to top