BISMILAH RAHMAN RAHIM
HAYA NDIYO MAAJABU KUMI ( 10 ) YA MCHANGANYIKO WA TENDE NA MAZIWA
Karibu Katika Makala hii Mahususi Ya Lishe Bora ambayo leo inakuangazia Umuhimu wa Juisi
ya Mchanganyiko wa TENDE na MAZIWA - Vyakula hivyo vinapoliwa kwa pamoja huwa ni
sawa na ‘dozi’ matata yenye kuwaongezea makali ya kuridhiana kinyumba baina ya wanandoa (
Mke Na Mume ).
Aidha, tende na maziwa huwa na uwezo pia wa kuwaondolea walaji uwezekano wa kupata
maradhi mbalimbali yakiwamo ya saratani na chanzo cha kuwa na uwezo huo ni wingi wa
virutubisho vinavyopatikana ndani ya mchanganyiko wa vyakula hivyo.
UNDANI WA MAAJABU 10
Kwa pamoja, baadhi ya virutubisho muhimu vinavyopatikana ndani ya mchanganyiko w
vyakula hivyo ni pamoja na vitamini B1, B2, B3, B5, A1 na C.
Vingine ni Calories (nishati) na madini yakiwamo ya Calcium, Potassium, Magnesium,
Phosphorous, kiinilishe cha Folate na pia wanga.
Mambo 10 ya faida yanayoweza kupatikana kwa ulaji wa mchanganyiko kama juisi ya tend
na maziwa kuwa ni pamoja na :-
MOJA
Kuwaongezea nguvu na ubora wa mbegu wanaume walio na tatizo hilo.
PILI
Kuinua hamu na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kwa kina mama; tatu kuimarish
afya ya mama mjamzito na kichanga chake.
NNE
Uwezo wa kusaidia kuondoa vilevi mwilini (hasa kwa wanywaji pombe).
TANO
Uwezo wa kuukinga mwili dhidi ya magonjwa kama saratani ya tumbo na kiharusi.
SITA
Kusaidia mchakato wa usagaji wa chakula tumboni.
SABA
Faida ya mchanganyiko huo kuondoa tatizo la ukosefu wa choo au mtu kupata cho
kigumu.
NANE
Uwezo wa kumuondolea mtu uchovu.
TISA
Kuongeza damu mwilini kutokana na kujaaliwa wingi wa madini chuma
KUMI
Uwezo wa kusaidia mishipa ya fahamu kufanya kazi yake vizuri.
Wanasayansi mbalimbali duniani wamebaini uwezo wa mchanganyiko wa tende na maziwa
katika kuupa mwili lishe muhimu na hivyo ni vyema kila mmoja kula vyakula hivyo kwa ajili ya
kuimarisha afya yake bila kujali jinsia.
Tende ina protini na hivyo faida hiyo huwa maradufu zinapoliwa kwa kuchanganywa na maziwa
ambayo pia yana protini kwa wingi.
Tende zina kiasi kidogo cha mafuta yasiyo na rehemu na protini yake inapokuwa na maziwa
huwasaidia watu wote , Yaani wanawake na wanaume, hasa katika masuala ya afya ya uzazi.
Mchanganyiko wa vyakula hivyo huwasaidia wajawazito kwa sababu huwa na madini ya chuma
kwa wingi na mjamzito anapotumia humfanya kuwa na kiasi cha damu cha kutosha na
mwishowe kuzaa salama na kuwa mwenye afya njema.
“Mchanganyiko huu humrahisishia mjamzito kuzaa salama kwa sababu tende ina sukari
ambayo huwapa nguvu wajawazito katika kusukuma mtoto wakati wa kujifungua… bila nguvu
uzazi huwa mgumu,” .
Tende husaidia kuondoa tatizo la ukosefu wa choo au mtu kupata choo kigumu kwa sababu
tunda hilo limejaaliwa kuwa na nyuzi nyuzi (fibers) ambazo husaidia uyeyushaji wa chakula na
hilo hufanyika vizuri kwa kula na maziwa.
“Pia huondoa uchovu mwilini kwa sababu ina virutubisho vya sukari asilia kama glucose,
sucrose na fructose,” .
Madini ya potassium yaliyomo ndani yake husaidia kumwepusha mtu na maradhi ya kiharusi na
ina kiasi kidogo cha chumvi ambayo husaidia kuimarisha mishipa ya fahamu.
“Tende husaidia kupunguza lehemu mwilini na kwa wale wenye matatizo ya ugonjwa wa
kukauka damu mwilini tende inaweza kuwapa ahueni kubwa,”.
“Tende ina vitamin A ambayo husaidia uoni mzuri na kuukinga mwili na maradhi, pia ina madini
ya chuma ambayo kazi yake ni kuzalisha chembechembe nyekundu za damu na ndiyo maana
zinapoliwa na maziwa huwa na msaada mkubwa kwa wajawazito.
MAANDALIZI.
Mchanganyiko wa tende na maziwa huweza kuandaliwa kwa namna nyingi na mojawapo ni
kuchukua tende zilizoiva kiasi cha kujaa kiganja kimoja cha mkono, kuondoa kokwa zake kisha
kuchanganya na glasi ya maziwa mabichi (fresh) kulingana na mahitaji.
Baada ya hapo, mchangayiko huo usagwe kwa pamoja ili kupata rojorojo kama juisi nzito
inayoweza kunywewa au kuwekwa kwanza kwenye friji ili ipate baridi kiasi Kidogo sana kabla
ya kutumiwa Ili Kufanya radha nzuri wakati wa Kutumia - Ujumbe huu nimeutayarisha
Mahususi Kwa ajili ya Kipindi hiki Cha Mwezi wa Ramadhani ambao Ndani yake Bidhaa Hii ya
Tende hupatikana Kwa Wingi Sana Na Si Mbali Na Maeneo tunayoishi , Tujitahidi Kudumu
Kwenye Matumizi ya Vitu Vya Asili ili kulinda Afya Zetu.
Wednesday, May 15, 2019
DARASA LA RAMADHANI
Bismillahi Rahmani Rahim. Karibuni wenzangu waumini wa kiislamu katika kipengele hiki kitachoelezea namna mama mjamzito na mama mnyonyeshaji mtoto watafunga Ramadhani yao.
✍๐ผ Eleweni enyi wenzangu kwamba, mwanamke mja mzito huwa hapati hedhi hivyo ni wajib kwake kufunga, Lakin pia mwenye kunyonyesha mtoto wake nae kama hayupo katika hedhi au nifasi ni wajib kwake kufunga.
๐ Lakini sasa , wawili hao wakichelea/wakihofia kwamba wakifunga watadhurika wao au wao na vitoto vyao vichanga basi hawatoruhusiwa kufunga , na watakuja kulipa swaumu zilizowafutu Siku zijazo baada ya mfungo .
๐ watalipa swaum ikiwa wamehofia madhara katika nafsi zao tu, na watalipa fidia pia kama itakua wamehofia madhara ya vitoto vyao vichanga . fidia hiyo ni kumlisha maskin au fukara mmoja kwa kila siku moja ambayo mtu hakufunga atamlisha maskini mmoja .
Allahu Aaalamu .
Katika kipemgele hiki tutizame namna gani mtu mzee yani Mtu mzima atatekeleza ibada ya swaum.
Mimi nawaomba muelewe enyi wenzangu wasaka Pepo ya kwamba, mtu yoyote mwenye kushindwa kufunga kwa sababu ya uzee anaruhusiwa asifunge na hatolipa swaumu Bali atatoa fidia tu ya kumlisha maskin mmoja ya kila siku ya Ramadhan.
Allahu Aaalamu .
✍๐ผ. Hadi hapo tuweke nukta.
☝yafahamuni vyema hayo
*WASAKA PEPO* (2019)
KAFARA LA KUFANYA TENDO LA NDOA KATIKA MCHANA WA RAMADHANI
Bismillahi Rahmani Rahim,
*KAFARA LA KUFANYA TENDO LA NDOA KATIKA MCHANA WA RAMADHANI*
✍Nawaomba mfahamu enyi wenzangu kwamba, kufanya tendo la ndoa kwa hiyari katika
mchana wa Ramadhani ni katika madhambi makubwa sana. Na sheria itamtaka mwenye kufanya
hivyo atoe kafara kubwa baada ya mfungo kuisha na kafara hiyo ipo katika utaratibu huu ufatao.
1)Kuacha mtumwa awe huru, hilo likishindikana afanye lifatalo.....
kisheria itabidi aanze upya kufunga hizo siku sitini kwa mfululizo. Ikishindikana hivyo atafanya
hili lifatalo
kwa kila siku moja utoe 2.5kg za chakula kwa maskini husika.
*MAELEZO YA ZIADA*
Kulipa kafara hiyo kuna ambatana na kulipa swaumu ya ile siku ambayo mtu alifanya tend
la ndoa katika mchana wa Ramadhani.
Ikiwa mwanamke kalazimishwa kufanya tendo la ndoa , hatolipa kafara atalipa swaumu tu
Lakin kama huyo mke naye alichochea kufanyika kwa tendo la ndoa mchana wa Ramadhani
atapaswa nae atoe kafara.
Wanandoa ambao ni wasafiri na hawakufunga na mtu ambaye amefanya tendo la ndoa kw
kujisahau , au ambaye alikua afahamu uharamu wa kufanya tendo la ndoa mchana wa
Ramadhani
Watu hao wakifanya tendo la ndoa mchana wa Ramadhani hawatalipa kafara Bali watalipa
swaumu tu .
Allahu Aaalamu.
Yafahamuni vyema hayo ☝
✍Hadi hapo tuweke nukta
*WASAKA PEPO* (2019)
RAMADHAN KAREEM.

- Kufunga siku sitini kwa mfululizo ila ikitokea dharula kama ya maradhi hatofululiza dharula
kisheria itabidi aanze upya kufunga hizo siku sitini kwa mfululizo. Ikishindikana hivyo atafanya
hili lifatalo
- kulisha masikini sitini kila mmoja 2.5kg cha chakula kinacholiwa Mara nyingi katika jamii
kwa kila siku moja utoe 2.5kg za chakula kwa maskini husika.
*MAELEZO YA ZIADA*
Kulipa kafara hiyo kuna ambatana na kulipa swaumu ya ile siku ambayo mtu alifanya tend
la ndoa katika mchana wa Ramadhani.
Ikiwa mwanamke kalazimishwa kufanya tendo la ndoa , hatolipa kafara atalipa swaumu tu
Lakin kama huyo mke naye alichochea kufanyika kwa tendo la ndoa mchana wa Ramadhani
atapaswa nae atoe kafara.
Wanandoa ambao ni wasafiri na hawakufunga na mtu ambaye amefanya tendo la ndoa kw
kujisahau , au ambaye alikua afahamu uharamu wa kufanya tendo la ndoa mchana wa
Ramadhani
Watu hao wakifanya tendo la ndoa mchana wa Ramadhani hawatalipa kafara Bali watalipa
swaumu tu .
Allahu Aaalamu.
Yafahamuni vyema hayo ☝
✍Hadi hapo tuweke nukta
*WASAKA PEPO* (2019)
RAMADHAN KAREEM.
SAWALA ZA USIKU
Basi Hili ni somo kuhusu swala za usiku, litakuwa katika sehemu 3
*SEHEMU YA KWANZA NI KATIKA KUZUNGUMZIA QIYAAMULLAYLI*
Fahamuni enyi wenzangu kwamba Qiyaamullayl ni swala ya sunnah yoyote inayoswaliw
usiku baada ya kuswali swala ya isha(swala ya sa mbili usiku) . Kisha fahamuni tena kwamba
idadi ya rakaa kwa swala hiyo ya qiyaamullayl ni rakaa mbili kisha watoa salamu. Hapo
namaanisha kwamba waweza swali rakaa zozote utakazo lakini kwa utaratibu wa kwamba
waswali rakaa mbili kisha watoa salamu alafu tena mbili kisha watoa salamu hadi pale
utapotimiza idadi ya rakaa ulizokusudia kuziswali.
Mfano wa Qiyaamullayli ni swala ya tarawehe.
Pia fahamu kuwa Qiyaamullayl waweza lala kwanza kisha ndo ukaamka kuiswali au waweza
iswali kwanza kisha ukalala.
*SEHEMU YA PILI NI KATIKA KUZUNGUMZIA TAHHAJUD*
✍Tahajjud ni aina ya Qiyaamullayl
yenye sifa moja kuu iliyo yamsingi.
Na sifa hiyo kuu ni kwamba tahajjud ni qiyaamullayli ambayo huswaliwa baada ya mtu kulala
kisha aka amka.
na hadi hapo tujikite katika sehemu ya tatu na ya mwisho inayohusu swala ya witri.
*SEHEMU YA TATU INAELEZEA KUHUSU SWALA YA WITRI*
Swala ya witri ni swala ambayo huswaliwa baada ya mtu kumaliza swala zake za usiku.
Witri inaweza swaliwa rakaa 1, 3 , 5, 7, 9 , 11.
Ukiiswali kwa rakaa tatu, utaswali mbili kisha utatoa salamu , alafu utasimama umalizie moj
ili ziwe tatu.
Ukiiswali kwa rakaa zozote zile katika hizo rakaa tulizotaja utaswali mbili mbili kisha moja y
mwisho utaiswali kivyake .
Pia katika rakaa ya mwisho ya swala hiyo ya witri ni vyema uombe dua ya qunuti ambayo
huombwa pindi unapotoka kurukuu sasa ukiwa umesimama wima kabla ya kusujudu, utaiomba
dua hiyo ya Qunuti ambayo nitaileta kwenu .
Twab-an.
Ndio kama hivyo. Na utaratibu wa swala zote hizo tulizozizungumzia ni kama ulele wa swal
nyingine yani swala tano za faradh kwa kuzingatia nguzo na masharti kama vile kuwa na udhu,
kuelekea qibla nakadhalika.
Na kwa hakika kuna thawabu, malipo na fadhila nyingi sana katika kuziswali swala za usiku
pamesemwa na waja wema kwamba swala hizo ni kifunguo cha kila kheri na kukubaliwa dua.
✍ Mpaka hapo tulipo fikia, nasema Allahu Aalamu, Assa laamu alaykum Warahmatullahi
Wabarakaatuhu.
Wasaka Pepo (2019)

Friday, May 10, 2019
YAJUE MAKUMI KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI
*1. KUMI LA KWANZA*
Hili ni kumi la *REHMA*
Uradi uliopendekezwa kusoma katika kumi hili ni: *YAA ARHAMA R-RAAHIMIYN*
IDADI ILIYOPENDEKEZWA NI 1,000 KILA SIKU
*NIA YA URADI:*
Ewe ALLAH uliyetukuka hakika nimetia nia ya kusoma uradi huu ili nipate radhi zako na unijaze rehma zilizopo katika kumi hili la mwanzo wa ramadhwaan. Nakuomba unikubalie ibada yangu hii kwako.
Ukijitahidi kufanya uradi huu mpaka ukamaluza kumi la mwanzo basi in shaa Allah utapata rehema zilizomo katika kumi hilo la mwanzo.
*2. KUMI LA PILI*
Hili ni kumi la *MSAMAHA* yaani kusamehewa madhambi yote yaliyopita.
Uradi uliopendekezwa kusoma katika kumi hili ni: *ASTAGHFIRULLAAH LA'ADHWIM WA ATUUBU ILAYHI*
IDADI ILIYOPENDEKEZWA NI 1,000 KILA SIKU
*NIA YA URADI:*
Ewe ALLAH uliyetukuka hakika nimetia nia ya kusoma uradi huu ili nipate radhi zako na unisamehe madhambi yangu yote niliyofanya kwa makusudi au kwa bahati mbaya naomba unipe radhi zako na msamaha wako uliopo katika kumi hili. Nakuomba unikubalie ibada yangu hii kwako.
*3. KUMI LA TATU*
Hili ni kumi la kuokolewa katika moto wa *JAHANNAM*
Uradi uliopendekezwa kusoma katika kumi hili ni: *ALLAHUMMA AJIRNAA MINA NNAAR SAALIMIYN*
IDADI ILIYOPENDEKEZWA NI 1,000 KILA SIKU
*NIA YA URADI:*
Ewe ALLAH uliyetukuka hakika nimetia nia ya kusoma uradi huu ili nipate radhi zako na uniepushe na adhabu za duniani na adhabu za jahannam nakuomba unikubalie ibada yangu hii kwako.
*MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KATIKA NYIRADI HIZO NI*๐๐ผ
1. Hakikisha unao UDHU.
2. Hakikisha unaelekea KIBLA.
3. Usikatishe uradi kwa ajili ya mazungumzo isipokua kwa dharura.
4. Chagua sehemu moja maalum ya kufanya nyiradi zako zote mpaka RAMADHAN itakapoisha. Labda itokee dharura kama KAZI,SAFARI, n.k.
5. Hakikisha baada kumaliza uradi kila siku kwa makumi yote omba dua ya shida zako na kisha mswalie Mtume (rehma na amani ziwe juu yake).
6. Muda mzuri wa kusomwa nyuradi hizi ni kabla ya kutoka adhana ya maghrib kwani muda huo ni muafaka kukubaliwa dua nyingi katika mwezi wa ramadhani. Ingawa inaruhusiwa kusoma nyuradi muda wowote.
Friday, May 3, 2019
RATIBA YA MASOMO
RATIBA YA KUJIFUNZA DINI KATIKA TAASISI YA WASAKA PEPO
Taasisi ya wasaka Pepo imewa andalia wanachama wake na waislamu wote ratiba ifatayo ya Masomo.
Baada ya swala ya Alfajir
๐ tutajifunza Qur-an tukufu.
Baada ya Swala ya Adhuhuri
๐ Kitasomeshwa kitabu cha (mabaadi-ul-fiqhiyyah)
๐ Hicho ni kitabu cha fiqhi/ Sharia.
Baada ya swala ya Alasiri
๐ Kitasomeshwa kitabu cha Al-ahaadiithul Mukhtaara.
๐ Ni kitabu cha hadithi za Mtume(s.a.w)
Baada ya swala ya Magharibi
๐ Kitasomeshwa kitabu cha (khulaaswatu nuuril yaqini)
๐ Hicho ni kitabu cha historia ya mtukufu wa Darja Mtume Muhammad(s.a.w)
Baada ya swala ya Ishaa-i
๐ kitafundishwa kitabu cha mawaaidhun baliighatun
๐ Hicho ni kitabu cha tazkia na uchamungu.
N:B
๐ Ratiba hiyo yaweza kubadilika kutokana na haja.
๐ Mahala pakujifunzia ni katika grupu ya taasisi iliyopo watsap
In sha Allah.
Twamuomba Allah atubaarik na atusahilishie katika masomo yetu
IMEANDALIWA NA AMIRI WA TAASISI YA WASAKA PEPO.
MUBACK HASSAN CHIZENGA
wasakapepo (2019)

Thursday, April 25, 2019
UBORA NA FADHILA ZA KUFUNGA MWEZI WA RAMADHANI
Hivi sasa tujifunze umuhimu, ubora, na fadhila za kufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
✍�� KUFUNGA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KUNA FAIDA ZIFATAZO.
�� Kunampatia muislam aliyefunga thawabu na radhi nyingi za Allah.
�� kunamuondoshea mtu aliyefunga madhambi ya siku za nyuma
�� Kuna mkinga muislam aliyefunga kutokana na moto,Maovu na madhila ya kiulimwengu.
�� kuna mjengea muislam aliyefunga moyo wa uvumilivu.
�� kuna mpelekea aliyefunga awe na tabia njema.
�� Kunaboresha afya ya mtu kwa kias kikubwa sana.
�� Kuna mfanya mtu awe mchamungu.
�� Kunamuondoshea mtu mawazo maovu.
*FAIDA ZA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI*
�� Ni mwezi ambao ndani yake milango yote ya pepo hufunguliwa.
�� Ni mwezi ambao ndani yake milango yote ya moto hufungwa.
�� Ni mwezi ambao ndani yake Mashetani wote hufungwa minyororo.
�� Ni mwezi ambao mambo mema hufanyiwa kawili yani malipo ya mema huzidishwa mar
nyingi zaidi.
kwa sasa tuweke nukta kidogo hapo hadi kesho mchana tutakapojifunza kuhusu mwanzo wa
kufunga kwa mwezi wa Ramadhani na mwisho wake in sha Allah.
Allahu Aalam.
Imeandaliwa na Amiri wa Taasisi ya Wasaka Pepo.
MUBARACK HASSAN CHIZENGA.

Subscribe to:
Posts (Atom)